

Utamaduni, Elimu ya Imani, Sanaa na Michezo ,
kumwezesha mtoto Kumudu stadi za kisanii, ubunifu na Michezo. Kuthamini utamaduni wa jamii yake, imani na tunu za taifa.
Eneo hili linajumuisha shughuli za kukuza na kuimarisha mwili ambazo hukuzwa kupitia shughuli za kisanii kama njia ya kuwasilisha ujumbe na ubunifu mbalimbali. Vilevile, eneo hili linamwezesha mtoto kutambua na kuthamini vitu vinavyohusiana na utamaduni wake kama vyakula, mavazi, sanaa za maonesho, na stadi za ubunifu zinazohusisha utendaji wa mwili ambao ni muhimu kwa afya njema. Mtaala huu unasisitiza watoto wajifunze imani zao ili kuwawezesha kujenga umahiri uliokusudiwa.
Kuonesha sanaa za maonyesho
Kubuni sanaa zinazohusisha utendaji wa mikono
Kutumia stadi za ubunifu zinazohusisha utendaji wa mwili
Kuthamini alama na tunu za taifa
Kuthamini vyakula vya Kitanzania
Kuthamini mavazi ya Kitanzania
Kuonesha matendo ya kiimani kulingana na imani yake
Kuheshimu imani za watu wengine
KITABU
MASOMO KATIKA PICHA & VIDEO
